Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Nyimbo ya Burna Boy kuimbwa wakati wa kuapishwa kwa BidenMsanii wa Nigeria Burna Boy amejumuishwa katika orodha ya miziki itakayochezwa wakati wa sherehe ya kuapishwa kwa rais mteule Joe Biden.Nyimbo ya Burna kwa jina Destiny itakuwa miongoni mwa nyimbo za wasanii wengine wa kimataifa.

Orodha ya nyimbo hizo 46 zimeandaliwa katika sherehe ya kuapishwa kwa Biden, taarifa hiyo imesema.

“Wasanii na nyimbo zilizochaguliwa ujumuisha taswira ya kila mmoja Marekani. Wanafungua ukurasa mpya na watasaidia kuleta watu pamoja wakati utawala wa Biden na Harris unaanza kazi yake muhimu ya kuunganisha nchi yetu,” taarifa hiyo imesema.

Nyimbo nyingine zilizochaguliwa ni pamoja na wasanii wakubwa kama BeyoncĂ© na nyimbo yake Find Your Way Back, Kendrick Lamar na Mary J. Blige‘s na wimbo wao Now Or Never, Bob Marley na Wailers na nyimbo yao Could You Be Loved pamoja na Levitating hit ya Dua Lipa.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments