Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Nyota wa Filamu toka Marekani, Tyrese Ameamua Kubadilisha DINI na kuwa Muumini wa dini ya Uislamu


Nyota wa filamu toka Marekani, Tyrese Darnell Gibson, @tyrese, maarufu zaidi kupitia filamu za Transformers na Fast & Furious, ameamua kubadilisha dini na kuwa Muumini wa dini ya Uislamu.


Kupitia ukurasa wake wa #Instagram, @tyrese amefunguka madhumuni na msukumo kuhusu msimamo wake wa imani, na kuelezea ya kua amezaliwa na kukulia katika misingi ya imani ya Kikristo lakini mara baada ya kwenda mataifa ya Mashariki ya kati ikiwemo taifa la Israel, alijikuta kusuasua kuhusu imani yake na huenda ikampelekea yeye kupata amani ya kuona dini ya Uislamu kumvutia zaidi.


"Men and women of faith! This is a powerful teachable moment so please be very alive in the comments," ameeleza.


Aidha, marafiki zake wanaamini kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 42, amekuwa akijifunza dini hiyo kwa muda mrefu na sasa ameamua kuslimu rasmi.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments