1/18/2021

Nyota Watatu Watemwa Simba
UONGOZI wa Simba umeamua kuachana na mpango wa kuwasajili nyota watatu waliokuwa wakifanya majaribio na timu hiyo kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi iliyomalizika Jumatano iliyopita.

 

Nyota hao ni Bernard Agele, Kelvin Moyo na Ian Nyoni ambao walikuwa miongoni mwa wachezaji walioifikisha Simba katika fainali ya michuano hiyo iliyofanyika visiwani Zanzibar.

 

Taarifa za uhakika zilizolifikia gazeti hili kutoka chanzo chetu ndani ya klabu hiyo, zimeeleza kuwa tayari nyota hao wameondoka jana asubuhi kurejea makwao.

 

“Agele kaondoka leo asubuhi (jana) na wengine wawili Moyo na Nyoni waliondoka usiku, aliyebaki ni mshambuliaji wa FC Platinum ya Zimbabwe, Perfect Chikwende, ambaye tayari usajili wake umefanyika na kutangazwa.

 

“Wale waliocheza Kombe la Mapinduzi wameondoka kutokana na kutolivutia benchi la ufundi, Chikwende anasubiri Ijumaa hii kujiunga na wachezaji wenzake kwa ajili ya mazoezi ya kujiandaa Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Afrika,” kilieleza chanzo chetu.

 

Alipoulizwa Kocha Msaidizi, Selemani Matola, alisema nyota hao walikuwa katika majaribio, hivyo lolote linaweza kutokea na uongozi utafuata mapendekezo ya benchi la ufundi kulingana mahitaji ya timu katika usajili.

 

“Walikuwa katika majaribio na viongozi wamesajili kulingana na mahitaji ya timu, tumemaliza Mapinduzi na tumerejea na tumewapa mapumziko ya wiki moja na Ijumaa hii tunaingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu na michuano ya kimataifa,” alisema Matola.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger