Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Padri Anayedaiwa Kubaka, Kumpa Mimba Mwanafunzi Afunguliwa Mashtaka UpyaALIYEKUWA Paroko wa Parokia ya Manushi Jimbo Katoliki la Moshi, Padri Erasmus Swai (44), ambaye anakabiliwa na kesi ya kubaka na kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha nne, amefutiwa mashtaka ya awali na kufunguliwa upya.


Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Nkamba Mbosela, jana Jumatatu, Januari 11, 2021, aliwasilisha hoja ya kuifuta kesi hiyo namba 159/2020 na kufunguliwa upya katika Mahakama ya Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro.


Padri Swai, anadaiwa kutenda makosa hayo kwa mtoto mwenye umri wa miaka 17 ambaye ni mwanafunzi wa sekondari, mkoani Arusha.


Akiwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama, Thurston Kombe, anayesikiliza kesi hiyo, Mbosela aliiambia mahakama kwamba upande wa mashtaka umebaini upungufu unaotokana na masuala ya kipelelezi.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments