Polisi Ainunulia Chakula cha Krisimasi Familia Moja Badala ya Kuikamata kwa Wizi wa Dukani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Afisa mmoja wa polisi ambaye alikua ameitwa kuikamata familia moja inayoshukiwa kuiba katika duka moja badala yake aliwanunulia chakula ili waweze kusherehekea chakula cha jioni cha Krismasi.

Matt Lima aliitwa katika duka moja la chakula katika eneo la Somerset , Massachussetts , mwezi uliopita , taarifa ya polisi ilisema.


Wanawake wawili walidaiwa kutoweka katika mashine ya skani vitu vyote walivyonunua katika duka hilo.


Walipoulizwa, familia hiyo ilisema kwamba haikuweza kulipia kila kitu walichokuwa wakihitaji kutokana na hali mbaya ya kiuchumi.


Hatahivyo walisema kwamba walikuwa wanafanya hivyo ili kuwatengenezea chakula kizuri cha krismasi watoto wao.


Bwana Lima aliwakamata lakini hakuwafungulia mashtaka kwa kuwa kila walichokuwa wamenunua kilikuwa chakula , polisi walisema.


Baadaye aliwanunulia kadi za zawadi zenye thamani ya $250 na fedha zake binafsi ili wanawake hao na watoto wao wawili kuweza kununua chakula cha krisimasi katika duka jingine la kampuni kama hiyo.


''Watoto hao wawili na wanawake hao walinikumbusha watoto wangu , hivyobasi nililazimika kuwasaidia'' , alisema afisa Lima.


''Ukweli ni kwamba familia hii ilikuwa inahitaji chakula hivyobasi siwezi kufikiria kufanya uamuzi kwenda katika duka la Stop and Shop na kununua kile ninachoweza kununua pekee - ama niende na kujaribu kununua chakula cha krisimamsi cha watoto hao''? aliambia runinga ya eneo hilo.


''Walinishukuru sana , mwanzo walikuwa wameshangaa. Nina hakika watu wengi walio katika hali hiyo wangefikiria kwamba kungekuwa na tukio tofauti na pengine wangekamatwa na kupelekwa mahakamani''.


''Nilinunua kadi ya thamani ya kile ambacho kingechukuliwa'', aliongezea.


''Nilifanya kile nilichoona ni sawa. Sio jambo la kunihusu nilijiweka katika viatu vya familia na kuonyesha huruma kidogo''.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad