Polisi Uganda wavamia kituo cha ukusanyaji wa kura kisicho cha serikali

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Polisi nchini Uganda wamevamia hoteli moja ambako kikundi cha wanaharakati wa mashirika ya kiraia na wakaguzi wa uchaguzi walikuwa wamekusanya taarifa kutoka kwa waangalizi wengine wa uchaguzi tofauti na Tume ya uchaguzi.
Msemaji wa polisi nchini humo, Bw Fred Enanga amesema kuwa walipata taarifa za ujasusi kwamba baadhi ya wanaharakati wa kiraia walikua wameweka kituo chao cha ukusanyaji wa matokeo ya kura katika Hteli Africana iliyopo mjini Kampala , kando na kituo cha taifa kinachokusanya matokeo ya uchaguzi wa rais na wabunge.

“ Tulituma watu wetu katika Hoteli Africana. Watu wenye jukumu la kudhibiti uchaguzi ni Tume ya uchaguzi. Huwezi kujua ni nini kilicho nyuma ya kituo hiki cha ukusanyaji wa matokeo ya kura. Huenda wana nia mbaya ambayo inaweza kuchochea ghasia . Sheria inaruhusu Tume ya uchaguzi tu kutangaza mataokeo. Kuwa na kituo cha kukusanya matokeo kando kunashusha hadhi ya uchaguzi na tume ya uchaguzi,” Bw Enanga aliiambia NTV Uganda.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hongereni Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa kufichua genge hili lenye nia
    ovu na lengo la kupotosha hatimae nchi iingie ktk machafuko.

    Asannteni kwa kuwadhibiti.

    ReplyDelete

Top Post Ad