Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Rais Ajitangaza Hadharani Kuambukizwa ‘Corona
 

RAIS wa Mexico, Andres Manuel Lopez Obrador,  kupitia akaunti yake ya Twitter ametangaza kupata maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya Corona usiku wa kuamikia leo.

 

Kwa muda mrefu kiongozi huyo amekuwa akiupuuzia ugonjwa huo na mara nyingi amekuwa akionekana hadharani pasipo kuvaa barakoa.  Katika ujumbe wake amesema dalili za ugonjwa huo si kali sana na kwamba anapata matibabu.

 

Ameongeza kwamba ataendelea na majukumu yake Ikulu ikiwa ni pamoja na kufanya mazungumzo ya simu ya Rais wa Russia, Vladimir Putin kuhusu chanjo iliyopatikana Russia ya ugonjwa huo iitwayo Sputnik V.

 

Mexico ni moja ya nchi 17 duniani ambazo zimeripoti matukio zaidi ya milioni moja ya Covid-19.

 

Idadi ya vifo na maambukizi vimekuwa vikiongezeka nchini humo tangu Oktoba mwaka jana na kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha Hopkins, Mexico imeripoti matukio zaidi ya  1,752,347 ya Covid-19 ambao umeua watu 49,084.


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments