Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Rais Magufuli: Shule ipo Dar Es Salaam wanafunzi wanakaa chini, Mkuu wa Wilaya yupo, Mkuu wa Mkoa yupo, Mkurugenzi wa Ubungo bado anakusanya kodi yupo na Mbunge wa Ubunge yupo tena ni profesa wa Elimu

 
”Kuna shule moja ya msingi Ubungo Dar Es Salaam inatwa Barango, ina wanafunzi wengi tu. Shule hiyo wanafunzi wapo Dar Es Salaam Ubungo bado wana kaa chini, madarasa mengine yamebomoka, madawati mengine yamevunjika yameachwa bure, Mkuu wa Wilaya yupo, Mkuu wa Mkoa yupo, Mkurugenzi wa Ubungo bado anakusanya kodi yupo na Mbunge wa Ubunge yupo tena yupo hapa na ni profesa tena wa Elimu, simama profesa wakuone kwenye jimbo lako, anafundisha elimu, mimi napenda kusema uwazi.” Rais Magufuli akifungua majengo ya shule ya sekondari ya Ihungo Kagera

”Lakini hiyo shule ya Ubungo Barango wanakaa chini, nina mshukuru huyo mwandishi ameitoa kwenye mitandao, viongozi wa kule wakaanza kusema ni maswala ya kisiasa, hayo sio maswala ya kisiasa hayo ndiyo ninayopenda kuyajua. Ninazungumza nikiwa Kagera lakini nikienda Dar Es Salaam niyakute hayo madarasa yamekamilika na wanafunzi hawakai chini, nitaenda kuitembelea hiyo shule kama wananisikia wa Dar Es Salaam ujumbe umefika.” Rais Magufuli akifungua majengo ya shule ya sekondari ya Ihungo Kagera


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments