Rais Trump Arejeshewa Akaunti Yake ya Twitter

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Rais wa Marekani, Donald Trump ameruhusiwa kuendelea kutuma ujumbe katika mtandao wa Twitter baada ya kufungiwa katika akaunti yake kwa saa 12. Akichapisha ujumbe wenye maudhui ya maridhiano, alijizuia kuchapisha madai ya uwongo kuhusu wizi wa kura.

 

Twitter ilisema kwamba itampiga marufuku kabisa rais Trumpiwapo atakiuka sheria za mtandao huo wa kijamii kwa mara nyengine. Hatua hiyo ya twitter inaweka wazi msimamo wake ikilinganishwa na facebook ambayo ilimpiga marufuku kwa muda mara moja siku ya Alhamisi. Badala yake Twitter imempatia rais huyo onyo la mwisho.

 

Mapema siku ya Alhamisi mtandao wa michezo wa twitch pia uliweka marufu katika akaunti ya Trumpambayo amekuwa akiitumia katika mikutano yake ya hadhara. Donald Trump aliandika ujumbe kadhaa Jumatano kwenye mtandao wa Twitter, na kuwaita waliovamia jengo la bunge la Capitol Hill “Wazalendo”. Pia alisema “Tunawapenda.”

 

Msemaji wa mtandao wa Twitter amesema: “Baada ya kuondolewa kwa ujumbe huo na kumalizika kwa zuio la kutumia mtandao huo kwa saa 12 ambalo alikuwa amewekewa, akaunti ya @realDonaldTrump imerejeshwa tena.

 

“Ukiukaji wowote wa sheria na kanuni za mtandao wa Twitter siku zijazo ikiwemo uadilifu au sera za vitisho vya vurugu, basi akaunti ya @realDonaldTrump itafungwa kabisa.”

 

Facebook

Awali hapo jana, rais alifungiwa kutumia akaunti ya Facebook na Instagram. Hatua hiyo itapitiwa tena baada ya Joe Biden kuapishwa rasmi kama rais wa Marekani, Januari 20. Mtandao huo wa kijamii awali ulikuwa umeweka marufuku ya saa 24 baada ya bunge la Marekani kushambuliwa.

 

Mkuu wa mtandao wa Facebook, Mark Zuckerberg, aliandika kuwa hatari ya kumruhusu Bwana Trump kuweka ujumbe mtandaoni “ni kubwa mno”.

 

Bwana Zuckerberg alisema Facebook iliondoa ujumbe wa rais “kwasababu tulihitimisha kwamba utakuwa na athari na kuna uwezekano mkubwa nia ikawa kusababisha vurugu zaidi”.

 

 

Alisema ni wazi kuwa Bwana Trump alidhamiria kushusha hadhi ya mabadilishano ya madaraka na rais mteule Joe Biden. “Kwahiyo, tunaongeza zuio la kutumia mtandao wa Facebook na Instagram kwa angalau wiki mbili zijazo hadi shughuli ya ubadilishanaji wa mamlaka kwa njia ya amani itakapokamilika,” aliandika.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad