Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Rais wa zamani wa Ghana kuzikwa leo
Kiongozi wa zamani aliyehudumu kwa muda mrefu nchini Ghana Jerry John Rawlings atazikwa siku ya Jumatano.
Mamia ya watu wametumia tangu siku ya Jumatatu kutoa heshima zao za mwisho.

Shughuli za mazishi zinafanyika huku kukiwa na hali ya kuzingatia masharti ya kupambana na virusi vya corona.

Bwana Rawlings aliaga dunia tarehe 12 mwezi Novemba katika hospitali ya Korle-Bu mjini Accra, baada ya kuugua kwa kipindi kifupi. alikuwa na miaka 73.

Akitambuliwa kuifanya Ghana kuwa thabiti, pia aliongoza utawala wa kijeshi kwa zaidi ya muongo mmoja kabla ya kurejesha nchi hiyo kwenye demokrasia ya vyama vingi mwaka 1992.

Pia alichangia jitihada za kutafuta amani nchini Liberia na Sierra Leone wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe katika miaka ya 1990 na hivi karibuni mjumbe wa Umoja wa Afrika nchini Somalia.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments