Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Saido Aanika Alivyoimaliza Simba Sc Akiwa Majeruhi
SAIDO Ntibanzokiza, kiungo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa wachezaji wenzake walimuomba awasaidie kuimaliza Simba, Januari 13 licha ya kuwa alikuwa na maumivu jambo ambalo alilifanya kwa kufunga penalti ya ushindi.

 

Ulikuwa ni mchezo wa kwanza kwa Ntibanzokiza ambaye ni ingizo jipya ndani ya Yanga kwenye usajili wa idirisha dogo akiwa ni mchezaji huru kwenye Kombe la Mapinduzi kwa kuwa kwenye mechi tatu hakuwepo kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

 

Yanga ilishinda kwa penalti 4-3 baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya bila kufungana jambo ambalo limeifanya Yanga kutwaa taji la pili la Kombe la Mapinduzi.

 

Mchezo wa fainali ulichezwa Uwanja wa Amaan ulishuhudiwa na mashabiki wengi waliojitokeza kuona mechi iliyokuwa na ushindani mkubwa.

 

Saido amesema:”Wachezaji wenzangu huwa ninawakubali na wao wananikubali, sasa walipoona mimi nipo na ninaweza kazi wakaniambia twende nami nikafanya kazi.

 

“Mchezo wangu dhidi ya Simba nilicheza licha ya kwamba bado nilikuwa nina maumivu ila nilifanya kwa ajili ya kazi na uwezo wangu mimi ni kucheza.” Yanga inatarajiwa kurejea leo na Kombe la Mapinduzi ambalo wamelitwaa visiwani Zanzibar.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments