Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Simba Kumtangaza Mpya Kocha Kesho, Yawaita TP Mazembe, Al HilalUONGOZI wa Klabu ya Simba umesema kuwa unakuja na mashindano mapya ya Simba Inter Cup ambayo yatashirikisha timu tatu ambazo ni Simba SC, TP Mazembe na Al Hilal ya Sudan ambayo yataanza Januari 27 hadi 31,2021.“Tunatangaza mashindano mapya ya SIMBA INTER CUP ambayo yatashirikisha timu tatu. Simba SC, TP Mazembe na Al Hilal ya Sudan. Mashindano yataanza Januari 27 hadi 31, 2021,” CEO Barbara Gonzalez.

 

“Kupitia mashindano haya Wanasimba watapata nafasi ya kuwaona wachezaji wapya na kocha. Kuanzia kesho tutatangaza watu ambao tumewaongeza katika benchi la ufundi,” amesema Manara.

  

Aidha, Klabu ya Simba imesema kuwa itamtangaza kocha Mkuu mpya na wachezaji wake wapya wakati timu yake itakapokuwa ikishiriki kwenye michuano ya Simba Inter Cup.

 

 

“Kesho tutamtambulisha kocha mpya na wasaidizi wake wawili pamoja na benchi la ufundi ambao wataiongoza timu kwenye mashindano mbalimbali. Kupitia mashindano ya Simba Super Cup, tutawatambulisha wachezaji wetu wapya kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa,” amesema Manara.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments