1/31/2021

Simba Mabingwa wa Simba Super CUP, Yawashukuru Mashabiki

 


MTENDAJI Mkuu wa Simba, (CEO) Barbara Gonzalez amesema kuwa mashabiki wanastahili pongezi kwa kujitokeza kwa wingi kuwashuhudia mabingwa wapya wa Simba Super Cup, Simba kwenye mchezo wa kilele cha mashindano hayo ambayo umemalizika leo Januari 31, Uwanja wa Mkapa.


Mashindano hayo ambayo yameshirikisha timu tatu ambazo ni Simba wenyeji, Al Hilal na TP Mazembe yalianza Januari 27 ambapo Simba walianza kwenye mchezo wa ufunguzi kwa ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Al Hilal.


Al Hilal ilishinda mabao 2-1 dhidi ya TP Mazembe Januari 29 Uwanja wa Mkapa na kujikusanyia jumla ya pointi tatu huku Mazembe wakiwa na pointi mbili wakiwa nafasi ya tatu.


Al Hilal ambao ni mabingwa wa pili pamoja na TP Mazembe wamepewa zawadi zao pamoja na medali Uwanja wa Mkapa.


Pia kulikuwa na zawadi ya mchezaji bora ambayo imekwenda kwa Rarry Bwalya huku mfungaji bora akiwa ni Bernard Morrison mwenye mabao mawili.


Luis Miquissone alikuwa mchezaji bora wa mchezo wa leo na kipa bora ametoka ndani ya Klabu ya Simba ambaye ni Beno Kakolanya akiwa amecheza mechi mbili na kufungwa bao moja.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger