Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Simba uso kwa uso na Namungo, Yanga yasubiri
KOMBE la Mapinduzi limefika patamu ambapo leo mchezo mmoja utachezwa Uwanja wa Amaan kati ya Azam FC dhidi ya Malindi kumsaka kinara wa kundi A ambaye atatinga hatua ya nusu fainali.  
Kundi hili ambalo litacheza leo ni C kinara wake kwa sasa ni Mlandege mwenye pointi mbili huku Azam FC ikiwa nafasi ya pili na Malindi ipo nafasi ya tatu zote zina pointi mojamoja. 

Mshindi wa leo atakutana na Yanga ambayo tayari imeshafunzu kwenye kundi B ambalo linaongoza ikiwa na pointi nne inafuatiwa na Namungo ambayo imeingia hatua ya nusu fainali kwa kuwa timu yenye matokeo mazuri, (best looser). 

Namungo ina pointi tatu baada ya kucheza michezo miwili, imefunga mabao mawili huku Mtibwa Sugar yenyewe ina pointi tatu ila imefunga bao moja.

Katika hatua ya nusu fainali itakayopigwa kesho Januari 11, 2021, Simba watakutana na Namungo huku Yanga wakimsubiri kinara wa Kundi C. 

Tayari bingwa mtetezi ambaye ni Mtibwa Sugar ameshavuliwa ubingwa na Simba baada ya kufungwa mabao 2-0 jambo lililomfanya abaki na pointi zake tatu na bao moja.Mchezo wa leo utachezwa majira ya saa 2:15 usiku.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments