Sukari ya Zuchu Yamfunika Nandy

advertise hereSECOND lady kutoka lebo kubwa ya muziki Bongo, Wasafi Classic Baby ‘WCB’, Zuhura Othman ‘Zuchu’ anazidi kutisha kisanaa.Taarifa ikufikie kwamba, kwa sasa mwanadada huyo anazidi kumfunika msanii mwenzake wa kike, Faustina Mfinanga ‘Nandy’.

 

ANAMFUNIKAJE?

Ishu nzima ni muziki ambapo hivi karibuni Zuchu alipakua ngoma yake mpya iitwayo Sukari ambao ulifanikiwa kuupiga kumbo wimbo wa Nandy unaosimama kwa jina la Number One.

 

Takwimu ziko hivi; wimbo wa Sukari umekuwa mtamu kwa watu na kutazamwa kwenye mtandao wa Youtube na mashabiki Mil1.8 ndani ya wiki moja.Idadi hiyo, imekuwa shubiri kwa wimbo wa Nandy, Number One ambao ndani ya wiki mbili umejikokota kwa kuwa na watazamaji Mil1.3 hadi wakati taarifa za stori hii zinakusanywa.ZUCHU HAKAMATIKI

Mbali na kuwa msanii aliyewika kwa muda mfupi ukilinganisha na Nandy ambaye kitambo amekuwa kwenye gemu, Zuchu ameweza kuweka rekodi ya kuwa msanii wa kike Afrika Mashariki mwenye wafuasi wengi (subscribes) kwenye mtandao wa Youtube.Rekodi hii ya kuwa na wafuasi wa kutosha kwenye mtandao huo ilikuwa ikishikiliwa na Nandy kabla ya kupigwa kumbo kibabe.

 

Kwa mujibu wa mtandao huo vita ya kimuziki imekolea zaidi kwa wasanii hao wa kike kwa takwimu zao kwenda zikichuana kama gemu ya Simba na Yanga.Katika siku za hivi karibuni Zuchu amefanikiwa kufikisha wafuatiliaji wake 700,000, akiwa amemuacha Nandy ambaye ana wafuatiliaji 648,000 kwenye mtandao huo.

 

NGOMA ZAO ZINAZOTIKISA ZAIDI

Miongoni mwa nyimbo za Zuchu zinazotazamwa zaidi kwa wakati huu ni pamoja na Raha, Wana, Nisamehe, Hakuna Kulala pamoja na Sukari ambayo kwa sasa ndiyo habari ya mjini.Nandy yeye anakimbiza zaidi na nyimbo kama Nusu, Kiza Kinene, Acha Lizame, Do Me na kamwe usiisahau hii mpya ya Number One.

 Nafasi za Ajira , Jiunge na Group Hili la TELEGRAM Usaidiwe Kutafuta Ajira Bonyeza HAPA Kujiunga


Hata hivyo, baadhi ya maoni kwenye mitandao ya kijamii yamekuwa wakipingana na mtazamo wa Zuchu kumzidi uwezo Nandy kimuziki kwa kile wanachodai msanii huyo anabebwa zaidi na ukubwa wa lebo yake ya WCB.

 

“Kumfananisha Zuchu na Nandy ni kumkosea heshima Nandy kwa sababu anapambana mwenyewe na kupata mafanikio ya kushangaza,” alisema mtoa maoni mmoja mtandaoni

GPL

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE