Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Tamko la Rais Magufuli kuhusu magonjwa ya mlipuko

 


Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli amesema licha ya uwepo wa magonjwa ya mlipuko kama Corona lakini watanzania hatutajifungia.

 

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Januari 27, 2021 alipokuwa akizindua shamba la miti la Chato lililopo wilayani Chato mkoani Geita.


''Nchi nyingi wamejifungia ndani, Watanzania hatujajifungia na hatutegemei kujifungia na wala sitegemei kutangaza kwamba tunajifungia ndani kwa sababu Mungu wetu yupo", amesema Rais Magufuli.


Aidha katika kuchukua tahadhari juu ya magonjwa ya mlipuko, Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli amesema watu waendelee kujifukiza na kuomba mungu pamoja na kufanya mazoezi.


Join Our Telegram Group for Job Updates CLICK HERE


"Tutaendelea kuchukua tahadhari za kiafya ikiwemo kujifukiza, huku tukimuomba Mungu, huku unapiga zoezi la kulima mahindi na viazi ili ule vizuri ushibe, Corona ashindwe kuingia kwenye mwili wako, mtatishwa sana lakini simameni imara", amesema Rais Magufuli.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments