Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Tanasha Awatoa Wanaume UdendaSTAA wa muziki kutoka nchini Kenya, Tanasha Donna, amewatoa udenda baadhi ya wanaume wakware ambao wamejikuta wakijiongezea machungu ya mwezi dume wa Januari.


Tanasha ambaye ni mzazi mwenza wa staa wa muziki barani Afrika, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ametupia picha yenye ‘hapetaiti’ kwa wanaume katika kurasa zake za mitandao ya kijamii za Facebook, Instagram na Twitter.

Picha hiyo inamuonesha Tanasha akiwa ameinama na kubinuka kiasi cha kulionesha sawia lile umbo lake kwa nyuma akiwa amevaa kigauni chepesi cha zambarau na bluu, kiasi cha kumchora dhahiri shahiri namna ambavyo nguo ya ndani imemkaa.


“Hii ndiyo maana halisi ya mwanamke tajiri…” Aliandika Tanasha kusindikiza picha hiyo tamu.Walichokifanya wanaume hao ni kummwagia sifa kuwa ni mwanamke mzuri huku wakimuomba awajibu DM (Direct Message) zao kwenye Instagram.

Mbali na hilo, baadhi ya mashabiki wake walimuita Diamond au Mondi kutembelea kurasa hizo ili kumuona Tanasha alivyonoga ambapo itamlazimu sasa hivi kurejesha majeshi kwake.

Hata hivyo, Tanasha ameendelea kuuchuna bila kuwajibu chochote. Tayari Tanasha aliyetengana na Mondi mwanzoni mwa mwaka jana amekuwa staa mkubwa wa muziki wa Afrika Mashariki.Ameanza mwaka huu wa 2021 vizuri kwa kuachia wimbo wake wa Kalypso ambao tayari umeanza kuweka rekodi Afrika Mashariki ukiwa na zaidi ya watazamaji laki 7 pale mjini YouTube ukishika nafasi za juu kabisa.


STORI; KHADIJA BAKARI, DAR

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments