Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Tanzia: Kigogo DART (Mwendokasi) Afariki DuniaALIYEKUWA Mkurugenzi wa Idara ya ya Maendeleo ya Usafirishaji, Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka – DART — maarufu kama Mabasi ya Mwendokasi, Mhandisi Charles Salus Ogare, amefariki dunia jana Jumatatu, Januari 25, 2021, majira ya saa 11: 00 asubuhi.


 


Taarifa iliyotolewa na Mtendaji Mkuu Wakala wa DART, Mhandisi Ronald Lwakatare, imesema kuwa,  Ogare amefariki dunia katika Hospitali ya Mloganzila jijini Dar es Salaam.


 


Mtendaji Mkuu Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka – DART Mhandisi Ronald Lwakatare anasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya ya Maendeleo ya Usafirishaji Mhandisi Charles Salus Ogare kilichotokea saa 11: 00 asubuhi Januari 25, 2021 katika Hospitali ya Mloganzila jijini Dar es Salaam.


 


Msiba upo nyumbani kwa marehemu Tabata Kinyerezi jirani na Songas jijini Dar es Salaam. Taarifa zaidi za msiba huu ikiwemo taratibu za mazishi zitatolewa baadaye.


 


Marehemu Ogare alizaliwa Machi 30, 1965, Mkoani Mara.  Mtendaji Mkuu anawaomba watumishi wote kushirikiana katika kipindi hiki kigumu cha msiba.


 


Raha ya Milele umpe Ee Bwana, na Mwanga wa Milele Umwangazie, Apumzike kwa AMANI, AMEN!

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments