Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Tanzia: Mwigizaji Mkongwe Nchini Marekani Afariki Dunia

 


#GetToKnow Mwigizaji mkongwe wa Marekani Cicely Tyson afariki dunia akiwa na umri wa miaka 96. Dunia itamkumbuka kama mwanzilishi kwenye tasnia ya uigizaji kwa upande wa Wanawake.


Chanzo cha kifo chake hakijatajwa. Tyson ametumia kipindi cha miongo Saba kwenye maisha yake kuigiza pia kufanya mitindo. Alikuwa mwanamke wa kwanza kucheza nafasi ya muhusika mkuu (main role) kwenye igizo la televisheni liitwalo East Side/West Side miaka ya 1960.


Kutokana na mafanikio yake makubwa kama mwigizaji wa Kike ikiwemo kupinga vikali nafasi za kibaguzi alizokuwa akipewa mwanamke kwenye uigizaji, mwaka 2016 Cicely alitunukiwa na Barack Obama medali ya uhuru inayotolewa na rais wa Marekani, ambayo ni ya juu kabisa ya kiraia.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments