Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Tetesi za soka kimataifa

Tottenham huenda ikamsajili beki mwenye umri wa miaka 22 raia wa Brazil Eder Militao - anayesakwa na Roma, AC Milan na Inter - kwa mkopo kutoka Real Madrid ikiwa na mbadala wa kumnunua kwa mkataba wa kudumu. (Corriere dello Sport - in Italian)
Klabu ya Jose Mourinho Tottenham Hotspurs imejiunga na Leeds na Juventus katika kumsaka winga wa klabu ya Stuttgart Nicolas Gonzalez, 22, huku mchezaji huyo wa Argentina akilengwa katika dirisha la uhamisho la majira ya joto. (The Athletic - subscription required)

Huenda pia kuna uhamisho mwengine kutoka Tottenham huku Valencia ikiwa na hamu ya kumsajili kiungo wa kati wa Spurs na England mwenye umri wa miaka 24 Harry Winks kwa mkopo . (Football London)

Brighton wana imani wameishinda Newcastle United katika kumsaini kiungo wa kati wa Ecuado Moises Caicedo kutoka klabu ya Indipendiente del Valle. Kinda huyo mwenye umri wa miaka 19 alikuwa akilengwa na klabu ya Man United(Talksport)

Kiungo wa kati wa Ufaransa na mshindi wa kombe la Dunia Steven N'Zonzi huenda mkataba wake wa mkopo katika klabu ya Rennes ukakatizwa baada ya kuhusishwa na uhamisho wa Arsenal na Everton . (Foot Mercato - in French)

Mshambuliaji wa Ufaransa na Lyon Moussa Dembele, 24, anakaribia uhamisho wa kuelekea Atletico Madrid baada ya kukataa uhamisho wa West Ham. (Telefoot via Sky Sports)

Arsenal hailengi tena kumsajili kiungo wa kati wa Norwich Emi Buendia baada ya klabu hiyo kuweka dau la £40m kumuuza mchezaji huyo wa Argentine. (Express)

Kiungo wa kati wa Chelsea Tiemoue Bakayoko anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo ya Stamford Bridge huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 akiendelea kuvutia klabu ya Napoli ambapo yupo kwa mkopo. (Star)

Beki wa Uholanzi Jetro Willems anaonekana huenda akarudi katika klabu ya Newcastle United kutoka klabu ya Eintracht Frankfurt, hatua hiyo inajiri baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kuhusishwa na kurudi katika klabu hiyo Tyneside. (Chronicle)

Leeds United imehusishwa na beki wa Norway anayetafutwa sana na Sampdoria mwenye umri wa miaka 22 Fredrik Andre Bjorkan. (La Repubblica via Yorkshire Evening Post)

Burnley inatarajiwa kuwasilisha ombi la kumsaini beki wa Everton mwenye umri wa miaka 23 Jonjoe Kenny, baada ya kushindwa hapo awali kumsaini mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya England ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 katika uwanja wa Turf Moor. (Football Insider)

Juventus ipo katika mazungumzo na klabu ya Sassuolo kuhusu uhamisho wa mshambuliaji wa Itali mwenye umri wa miaka 22 Gianluca Scamacca, ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Serie A Genoa. (Goal)

Burnley inatarajiwa kuwasilisha ombi la kumsaini beki wa Everton mwenye umri wa miaka 23 Jonjoe Kenny

Beki wa RB Leipzig na Ufaransa Dayot Upamecano, 22, anatakiwa na klabu ya Bayern Munich, huku klabu hiyo ya Bundesliga ikijiunga na Chelsea na Manchester United katika kumtafuta beki huyo.. (Marca)

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments