Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Trump Aaanza Maisha Mapya ‘Uraiani’

 ALIYEKUWA Rais wa Marekani, Donald Trump, ameanza maisha ya kawaida kama raia wengine akiwa katika uwanja wake wa golfu huko West Palm, wakati Spika wa Bunge, Nancy Pelosi, akifurahia kuondoka kwake jijini Washington.


 


Rais huyo wa zamani anapenda kucheza golfu na mara nyingi alikuwa akiutumia muda wake wa mapumziko akiwa huko Florida, New Jersey au kwenye vilabu vyake vingine duniani.


 


Trump alikuwa amevaa kofia yake ya kawaida iliyoandikwa ‘Make America Great Again’ wakati akicheza mchezo huo na kusindikizwa uwanjani huko na magari ya serikali kutoka kwenye klabu yaka ya Mar-a-Lago ambayo ndiko nyumbani kwake na mkewe Melania.Pia aliyeonekana huko Mar-a-Lago alikuwa ni Lara Trump, akiwa amevaa kivazi maalum cheupe cha kuogolea.


Lara ameolewa na Eric, mtoto wa Trump ambapo mwanamke huyo anadaiwa atagombea kiti cha useneti huko  North Carolina mwaka 2022.


Wakati huohuo, Pelosi alisema: “Rais alifanya kitendo cha uchochezi na vurugu.  Sidhani kama ni kitendo cha kuleta umoja,  hata hivyo, tulisahau jambo hili.  Kitendo hicho si cha kuleta umoja.”


Alikuwa akizungumzia kitendo cha watu waliovamia bunge (Capitol Hill) na katika tafrani iliyofuatia watu watano waliuawa.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments