Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Tume ya Ushindani Yaanza Uchunguzi Mabadiliko Simba

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE
TUME ya Ushindani (FCC) imeanza uchunguzi wa mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu ya Simba ambao unawahusu wadaawa watano.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na FCC kwenye Gazeti la Serikali la Daily News leo Januari 15, 2021, wadaawa hao ni Simba Sports Club Holding Company Limited ambaye ni mdaawa wa kwanza, Mo Simba Company Limited (Mdaawa wa pili), Simba Sports Club Company Limited, Simba Sports Club na Mohammed Gulamabbas Hassanali Dewji.

 

Taarifa ya FCC imesema kuwa mdaawa wa tatu kwa kushirikiana na mdaawa wa kwanza, pili na tano walichukua mali na biashara za mdaawa wanne Tanzania Bara bila kuitaarifa tume hiyo kinyume na sheria ya ushindani kifungu cha 11 (2), 11 (6) (cha mwaka 2018) na kizingiti cha muunganiko wa makampuni cha mwaka 2017.“Januari 6 mwaka huu, FCC ilifanya maamuzi kwa kutoa matokeo ya awali kuhusiana na tuhuma zinazowakabili wadaawa wote watano.

 

“Kitendo cha wadaawa wote watano kushindwa kuitaarifu FCC juu ya muunganiko huo wa makampuni kilisababisha kuinyima tume hiyo nafasi ya kutekeleza jukumu lake la kisheria la kufanya tathmini juu ya uhalali wa muunganiko huo unaotuhumiwa kutotaarifiwa kwake kwa mujibu wa sheria,” imesema taarifa hiyo.

 

Tume hiyo pia imetoa nafasi mtu, kampuni, shirika au taasisi kuwasilisha pingamizi kwa kuwa na sababu za kuaminika kuwa muunganiko unaotuhumiwa kutekelezwa na wadaawa wote watano bila kutolewa taarifa kwa FCC kumeathiri au unaweza kuathiri maslahi yake.

 

Kwa upande wake, mwanasheria wa klabu ya Simba, Mhina M. Mhina alikiri kupokea taarifa hiyo kutoka FCC na wanaandaa taarifa rasmi.

 

“Tunaandaa taarifa kuhusiana na suala hilo, na msemaji wa klabu ataitangaza kwa mujibu wa utaratibu wetu,” alisema Mhina kwa njia ya simu.


Post a Comment

0 Comments