Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Tusaidiane Kutafakari Kauli Zenye Utata za Mama Diamond Platnumz Kuhusu Mzee Abdul Kuwa Si Baba wa Mondi


HABARI zilizoshtadi mjini kwa sasa ni kadhia ya mama Diamond kumkana baba Diamond (mzee Abdul) kwa idhlali na taadhira kubwa, kuwa si baba mzazi wa Diamond. Naam hii ni HABARI. Na sisi (kwenye balagha) tunasema hivi:

Yaani kwa ufupi: HABARI ni maneno yanayopelekea UKWELI na/au UONGO kutokana na uthibitisho wake. Kwahiyo, sifa ya HABARI yoyote ile duniani, ni kubeba taarifa ya KWELI au ya UONGO. Sasa, utajuaje kwamba HABARI flani ni ya KWELI au ya UONGO? Wanazuoni wa Balagha wanafafanua:


1. Mama Diamond anasema kuwa, mzee Abdul hakuwa baba mzazi wa Diamond, inakuaje tena (yeye huyo huyo) aseme kwamba, mzee Abdul aliikataa mimba? Alikataaje kitu (mimba) ambacho si chake? Na kama ni kweli ALIIKATAA, maana yake ni kwamba, basi mama Diamond alitaka kumpa hiyo mimba. Kwanini alitaka kumpa kitu (mimba) ambacho siyo chake? Kwa lugha rahisi alitaka KUMBAMBIKIA). Je, kosa la mzee Abdul ni kukataa kubambikwa?

Hili swali naomba walijibu watoto wa darasa la pili kwa sababu ni jepesi sana. Lakini maswali yanayofuata sasa ndo naomba yajibiwe na watu wazima:


2. Mama Diamond amesema kwamba, mzee Abdul hakuwa baba mzazi wa Diamond—alikuwa ni baba mlezi tu. Pia, yeye huyo huyo akasema tena kuwa, mzee Abdul aliahidi kumlea Diamond lakini HAKUMLEA (rudia hilo neno—HAKUMLEA). Na hata yeye (mama Diamond) hakuwahi kuishi kwa mzee Abdul—na hata picha walizoonekana wakiwa pamoja (kipindi Diamond akiwa mtoto), ilikuwa tu wamepita kumsalimia mzee Abdul hapo Magomeni alipokuwa akiishi.

Swali: Je, mtu ambaye umesema hakuwa baba mzazi wa mtoto, na umesisitiza kuwa HAKUMLEA, hicho cheo cha "BABA MLEZI" kilitoka wapi? Alikuwa analea nini?


3. Mama Diamond amesema, mzee Abdul alikataa mimba (ubaya), lakini pia amesema, hakuwa akihudumia kama alivyoahidi (ubaya), pia amesisitiza kuwa, mimba haikuwa yake (ubaya). Kwa lugha rahisi, mama Diamond ameamua kumpaka UBAYA mzee Abdul. Swali: Kama hayo ni kweli, je, hizo pesa ambazo mama Diamond alikuwa anapewa mara kwa mara na Diamond ili akampatie mzee Abdul zilikuwa zinakwenda kwa mzee Abdul kama nani? (Maana mtoto hakumzaa yeye, na wala hakumlea).


4. Mama Diamond amesema, alimpa Diamond ubini wa Abdul kwa sababu (mzee) Abdul ndiye aliyempeleka hospitali kujifungua. Pamoja na hayo, amesisitiza kuwa bwana Salum Nyange (anayemtaja kuwa ndiye baba mzazi wa Diamond), alikuwa anakwenda Tandale kumangalia mtoto (Diamond) kama kawaida. Maana yake ni kwamba, mzee Salum Nyange hakumkataa mtoto. Swali: Inawezekanaje mtu yule yule (mzee Abdul) aliyetaka kubambikwa mimba akaikataa, ndiye akasimama kidete kumpeleka mama Diamond hospitali? Kama mwenye mimba (Salum Nyange) alikuwepo na hakukataa mimba, ilikuwaje mama Diamond ampe mtoto (Diamond) u-bini wa mtu mwingine (mzee Abdul) kisa tu alimpeleka hospitali kujifungua? Je, ilikuwaje mzee Abdul akaahidi KUMLEA Diamond ilhali baba mzazi wa Diamond (bwana Salum Nyange) alikuwa hai na alikuwa anakwenda kumwangalia mtoto?

Download App ya Udaku Special HAPA Kusoma Hizi Habari Kupitia Simu yako Kirahisi


Somo la HABARI Kibalagha ni pana sana. Tungeweza kwenda mbali zaidi, kwa kuangalia, je, HABARI iliyoletwa na mama Diamond ilikuwa ni HABARI ya awali yenye kutoa taarifa (الخبر الابتداىي), au ilikuwa ni HABARI ithibitishayo taarifa yenye mashaka (الخبر الطلبي), au ilikuwa ni HABARI yenye kusisitiza jambo lililobishiwa ( الخبر الاءنكاري)?


Ukimsikiliza mama Diamond, anasisitiza kuwa hata mzee Abdul mwenyewe ANAJUA kwamba si baba mzazi wa Diamond. Msisitizo huu unaonesha kwamba habari/maneno hayo yaliwahi KUBISHIWA ( الخبر الاءنكاري). Lakini, ukimsikiliza mzee Abdul, muda mfupi baada ya mahojiano aliyofanya mama Diamond, utamsikia akisema: HABISHI kuwa yeye si baba yake Diamond. AMEKUBALI baada ya kusikia kauli ya mama Diamond. Siku zote hakuwa na YAKINI juu ya hili. Kwa hivyo, hii ni habari mpya kwake (الخبر الابتداىي). Swali: kwanini mama Diamond alitumia MKAZO kana kwamba baba Diamond aliwahi kubishia HABARI hii ( الخبر الاءنكاري)?


Kwa kutumia NYENZO za balagha ili kupambanua habari hii, nadhani kila mmoja anaweza kuja na majibu yake bila kutaghadhabu. Mimi nimechochea TAFAKURI tu—na mpira nimeuacha kwenu.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

2 Comments

 1. Huu ni mchezo wa Esma na Juma Lokole ndio waliompeleka mama Darasani.

  Mwenyee akili haambiwi Rudia Kuitazama Intaview. Dida ameshiriki

  na hata kambla ya mamaa kupatikana na kujibu mpango mzima Alieropoka
  Jibu na ambazo ndiyo inakuja kuwa kauli ya mama hewani ni Juma.

  Sasa ukitaka kujua Fikira na mpango ulianzia wapi? Mshikilieni Juma na Esma hii yote ilianza baada ya tofauti za MwanaHawa ndani ya nyumba na Esma ndio mchongo uliponza na baada ya talaka na mimba kudondoshwa matokeo ndio huu Usani na new muvi.

  Mzee Abduli ana haki ya kufungua mashtaka ya Moral na mental anguish civil compensation . Hiyo ikiwa hamjampa B.P na Sukari. Mzee halali kwa sasa
  na amesha anza kudhohofika na Msongo wa Mawazo kwa betrayal ya Sanura.

  ReplyDelete
 2. Huu ni mchezo wa Esma na Juma Lokole ndio waliompeleka mama Darasani.

  Mwenyee akili haambiwi Rudia Kuitazama Intaview. Dida ameshiriki

  na hata kambla ya mamaa kupatikana na kujibu mpango mzima Alieropoka
  Jibu na ambazo ndiyo inakuja kuwa kauli ya mama hewani ni Juma.

  Sasa ukitaka kujua Fikira na mpango ulianzia wapi? Mshikilieni Juma na Esma hii yote ilianza baada ya tofauti za MwanaHawa ndani ya nyumba na Esma ndio mchongo uliponza na baada ya talaka na mimba kudondoshwa matokeo ndio huu Usani na new muvi.

  Mzee Abduli ana haki ya kufungua mashtaka ya Moral na mental anguish civil compensation . Hiyo ikiwa hamjampa B.P na Sukari. Mzee halali kwa sasa
  na amesha anza kudhohofika na Msongo wa Mawazo kwa betrayal ya Sanura.

  ReplyDelete
Emoji
(y)
:)
:(
hihi
:-)
:D
=D
:-d
;(
;-(
@-)
:P
:o
:>)
(o)
:p
(p)
:-s
(m)
8-)
:-t
:-b
b-(
:-#
=p~
x-)
(k)