Unaambiwa Penzi la Kanye West na Kim Kardashian limefikia Mwisho...Wapeana Talaka Tatu

 


Penzi la Kanye West na Kim Kardashian limefikia mwisho, wameripotiwa kuachana baada ya kukaa kwenye ndoa kwa miaka 6. Vyanzo mbali mbali vimeiambia tovuti ya Page Six kwamba talaka tayari imetolewa na wawili hao wameachana rasmi.


"Wanafanya kimya kimya lakini ndio wameshamalizana. Kim ameajiri mwanasheria wa talaka Laura Wasser na wapo kwenye mazungumzo ya namna ya kumalizana." kilisema chanzo hicho.


Kim Kardashian (40), hajaonekana kuvaa Pete ya ndoa katika kipindi cha hivi karibuni na Kanye West (43), ameendelea kubaki mjini Wyoming katika kipindi chote cha Sikukuu badala ya kuutumia muda na familia yake. Taarifa zingine zinasema walikuwa wakiishi kila mmoja kivyake miezi michache iliyopita.HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments