Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Unaambiwa Rapper EMINEM Baada ya Kupona Uteja wa Madawa ya Kulevya Ilipidi Ajifunze Upya Kurap, Afunguka Issue ya Kumchana Rihanna


Eminem aliwahi kupitia kipindi kigumu cha uteja wa dawa za kulevya, urahibu ule ulipelekea ajifunze kuchana (Ku-Rap) upya mara baada ya kupona. Eminem amefunguka hayo wakati akijadili sakata la kumchana Rihanna kwenye moja ya mistari yake kipindi ambacho amepigwa vibaya na Chris Brown


Kwenye ngoma hiyo, Eminem alichana "Bila shaka nipo upande wa Chris Brown, ningempa kipigo yule kahaba pia." ilisikika mistari ya Eminem kwenye ngoma hiyo iliyovuja.


Sasa wakati akiiongelea, alisema hicho ndio kipindi ambacho alikuwa akijifunza ku-rap tena mara baada ya kupitia urahibu wa dawa za kulevya, na mistari hiyo aliiandika wakati akinoa upya makali ya kichwa chake kiuandishi.


"Ni miaka 10 na zaidi imepita, lakini siwezi kuomba radhi kwa hilo. Nilisema na sikuwa sahihi kusema vile. Ulikuwa ni upumbavu. Unajua mara nyingi hasa hasa katika kipindi cha kuandika 'Relapse' pale nilipoanza kujifunza kuchana tena, kwa sababu ya hali yangu ya dawa za kulevya niliyopitia na kunifanya kujifunza upya vitu vingi. Na hicho ni kimojawapo." alisema Eminem kwenye mahojiano na Gray Rizzy wa SiriusXM, Shade 45.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments