Unaambiwa TELEGRAM Yazidi Kupanda Chat Baada ya Whats App Kutaka Maelezo ya Faragha...Waingiza Watu Mamilioni 25 ndani ya Masaa 72

Hivi karibuni kumekuwa na mijadala mtandaoni kuhusu Sera Mpya ya Faragha ya WhatsApp ambayo itaanza kutumika Februari 8 huku watu wengi wakisema kuwa huo ni mwisho wa faragha ya watumiaji wa WhatsApp


Tajiri namba moja duniani Elon Musk aliwataka watu wahamie Mtandao wa Signal kwa madai una Sera nzuri ya Faragha kuliko WhatsApp


Aidha, Mtandao wa Signal umeripoti kupata maombi mengi ya waliojiunga kwa mara ya kwanza katika mtandao huo. Hata hivyo imeonekana pia kuwa fursa kwa mitandao mingine inayofanya kazi sawa na WhatsApp


Mtandao wa Telegram umeripoti kuwa na watumiaji walio 'active' zaidi ya milioni 500, huku wakiwa wamepata watumiaji wapya zaidi ya milioni 25 ndani ya saa 72

That Gal ya Rosa Ree Yawa Gumzo Itazame Hapa chini:

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments