Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Undani wa Shule atayoizindua Magufuli leoRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anatarajia kuzindua shule ya sekondari ya wavulana Ihungo iliyoko mjini Bukoba ambayo imejengwa upya mara baada ya kuathiriwa na tetemeko la ardhi.


Rais Magufuli atazindua shule hiyo leo, 18/01/2021 sambamba na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa chuo cha VETA ikiwa ni muendelezo wa ziara yake aliyoanza jana katika mkoa wa Kagera.


Shule  ya wavulana Ihungo  imefanyiwa ukarabati  uliogharimu shilingi Bilioni 10.9 baada ya kuharibika kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea mjini Bukoba tarehe 10 Septemba, 2016.


Rais Magufuli yuko ziarani katika mkoa wa Kagera ambapo anatarajia kuzindua miradi mbalimbali pamoja na kushuhudia utiaji saini wa mradi mkubwa katika mkoa huo wa madini ya Nickel yanayopatikana maeneo ya Bugarama, Wilaya Ngara ambao utanufaisha vijana katika mkoa huo

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments