Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Usalama waimarishwa katika majengo ya bunge UjerumaniGazeti la Ujerumani la Bild limeripoti kuwa polisi imeimarisha usalama katika majengo ya bunge ya Ujerumani mjini Berlin kufuatia uvamizi uliotokea katika majengo ya bunge nchini Marekani.

Protesters and police outside the Reichstag 

Gazeti hilo limenukuu barua ya Rais wa Bunge la Ujerumani Wolfgang Schaeuble kwa wabunge nchini humo. Schaeuble ametaka ripoti kutoka ofisi ya wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani juu ya ghasia zilizotokea katika majengo ya bunge nchini Marekani na kuwa serikali itatoa maelekeo zaidi na mafunzo watakayoyapata katika uvamizi wa Marekani ili kulilinda bunge.

Mnamo siku ya Alhamisi, msemaji wa polisi alisema watachukua hatua zaidi ili kuimarisha usalama katika majengo muhimu mjini Berlin, akiashiria jengo la Reichstag lenye makao ya bunge ya Ujerumani na sehemu zenye mafungamano na Marekani.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments