Video za Ngono Zamwondoa Uhai Mrembo Huyu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Pengine haikuchukua muda mrefu kwa Tiziana Cantone kuanza mfululizo wa matukio ambayo yalisababisha kujikatisha uhai.

 

Mwezi Aprili mwaka 2015, mwanadada kutoka Mugnano, nje kidogo mwa Naples, alituma picha za video za ngono kupitia WhatsApp. Waliopokea video hizo miongoni mwao ni rafiki yake wa kiume Sergio Di Palo, ambaye mahusiano yake naye hayakuwa mazuri.

 

Video hizo zilimuonesha Tiziana akifanya vitendo vya ngono na wanaume kadhaa ambao hawakufahamika. ”Alikuwa mrembo lakini mwenye kuvunjika moyo upesi,”alikumbuka Teresa Petrosino ambaye walikua marafiki kwa miaka 15.” Alikuwa na watu wasiofaa kwa wakati usiofaa.”

 

Video hizo zilisambazwa kwenye tovuti mbalimbali zinazoonyesha masuala ya ngono. Vitendo vyenyewe kwenye video hizo havikua kitu isipokua sentensi moja tu kutoka mdomoni mwa Tiziana Conte. ”Unarekodi video?” alimuuliza mwanaume aliyekuwa ameshika Kamera. ”Safiiii”.

 

Maneno hayo yaliashiria kuwa mwanadada huyo anapenda kupigwa picha wakati akifanya ngono. Sentensi hiyo ilifanya watazamaji waendelee kuitazama bila wasiwasi. Kama alikua anafurahia kupigwa picha, bila shaka hatachukia watu wakiitazama.

 

Lakini waitaliano walifanya zaidi ya kutazama.Watazamaji walitumia maneno yake kwa msisitizo wakatengeneza t-shirt ambazo ziliwekwa picha yake na pia kwenye tovuti. Hakuna aliyekuwa akifikiria kuwa Tiziana asingependa, kwa kuwa alionekana kufurahia kwenye video hizo.

 

Lakini mambo hayakua hivyo

”Watu huchanganya kukubali jambo na jambo hilo kusambaa zaidi,” anaeleza mtaalamu wa masuala ya mitandao Selvaggia Lucarelli.

”Unaweza kupiga picha ya video, ukawaonesha watu kadhaa,lakini kunakua na makubaliano kuwa watu hao wasisambaze zaidi.”



Mapambano ya kisheria

Tiziana Cantone, aligopeshwa sana na hali hii. ”Mimi na yeye hatukuwahi kuongea kuhusu kilichomo kwenye video.” alisema rafiki yake Teresa.”Sikuwahi kuziona, na sikutaka kuziona.Unaweza kuona alikuwa akisumbuka mno.”Lakini alikuwa na nguvu.”

 

Bi Cantone akaamua kupambana.Lakini hakukua na njia ya haraka ya kufanya ili kuondosha video hizo. Aliipeleka kesi mahakamani, akidai kuwa video hizo zilipelekwa kwenye mitandao bila ridhaa yake.Lakini mpaka wakati huo hakuweza kuishi maisha ya kawaida.

 

”Hakutaka kutoka nje akiogopa watamuona.” Alieleza Teresa. ”Alielewa kwa kiasi fulani kuwa hali hii haiwezi kutatulika;kuwa mume wake,watoto wake wanaweza kuziona video hizo siku moja;na kuwa video hizo hazitaondoka mitandaoni.”

 

Ilimchukua wiki kadhaa Mama yake Teresa Giglio kupata nguvu kuwaambia wanahabari kuhusu maisha ya binti yake. ”Binti yangu alikua na tabia njema lakini pia alikua na mapungufu yake,” aliiambia BBC. ”Hakua na mapenzi ya baba, tangu alipozaliwa.Hakuwahi kumuona baba yake.Hii iliathiri maisha yake.”

 

Mama na mwana waliishi pamoja.Katika kipindi cha furaha, Tiziana alipenda kusikiliza wanamuziki wa Italia, kusoma vitabu vya simulizi, kupiga kinanda.Lakini baada ya video kutapakaa mitandaoni hali hiyo haikuwepo tena.
”Maisha yake yaliharibika, mbele ya kila mtu,” alisema mama yake.”Watu walimfanya kichekesho,akaitwa majina mabaya ya aibu.”

 

Mwezi Septemba, Mahakama ya Naples iliamuru video hizo zitolewe mitandaoni na kwenye tovuti.Lakini ilimtaka Tizianz alipe faini ya dola 21,600 za marekani, gharama za huduma za kisheria.Fedha ilikua nyingi sana. Tarehe 13 mwezi Septemba mwaka 2016, Maria Teresa Giglio alikwenda kazini, akiwa amemuacha binti yake nyumbani.

 

Bi Giglio alipokea simu kutoka kwa wifi yake ,sauti ikiwa ya kupoa sana ikimtaka arejee nyumbani. Aliporejea alikuta Polisi, gari ya kubeba wagonjwa, ”haraka nikaelewa”alisema , huku akilia. ”Siku alipokufa maisha yangu yalikomea hapo.”



Nani aliweka video Mtandaoni?

Kitendo cha Tiziana Cantone kujitoa uhai, kilifanya video hizo zifuatiliwe na watu wengi zaidi kuliko kusahaulika. Mama yake alijilazimisha azitazame video hizo.

 

”Nilitaka kuona kila kitu ili niweze kuuelewa ukweli.” huyu hakua Tiziana wangu” alishawishika kuwa binti yake alikua anatumia dawa za kulevya.

 

Bi Giglio amemtaka mpenzi wa zamani wa binti yake, Di Pialo, kueleza hasa alishiriki vipi katika mpango wa kusambaza video zile. ”Hakunisaidia kuokoa maisha yake.Lakini labda anaweza kunisaidia kupata ukweli.

 
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad