Vifo vinne vya ajali vyatikisa Moshi Mwaka Mpya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Moshi. Ni simanzi na majonzi mjini hapa kutokana na vifo vya watu wanne vilivyotokana na ajali siku ya Mwaka Mpya.


George Jamal maarufu kwa jina la George Washington alifariki juzi akitibiwa Hospitali ya Rufaa ya KCMC wakati Jackson Kisamo maarufu kwa jina la mkata umeme na wenzake wawili walifariki juzi asubuhi pia.


Vifo hivyo vimekuwa gumzo kutokana na kutokea siku ya Mwaka Mpya na vyote vikisababishwa na ajali kati ya mabasi na pikipiki zilizokuwa zikiendeshwa na Jackson na George Washington.


Jambo jingine linalofanya vifo hivyo kuwa gumzo ni kuwa pikipiki iliyokuwa ikiendeshwa na Jackson, walimu wawili aliokuwa amewapakia nao walipoteza maisha katika ajali hiyo.


Mbali na mazingira hayo, Jackson na walimu hao wawili wote wanaishi mtaa mmoja wa Mdawi wilayani Moshi na wakati walimu hao wakielezwa kuwa ni ndugu, mtoto wa baba mkubwa na mdogo.


Picha za George na Jackson zimekuwa zikisambaa kwa kasi kuanzia juzi kutokana na umaarufu waliokuwa nao kwa jamii.

 

“George Washington pumzika kwa amani brother. Duh,” aliandika mmoja wa wachangiaji katika mtandao wa kijamii na mwingine akiandika “Yesuu mkata umeme amekufa. Sijaamini bado. Duniani tunapita”.


RPC Kilimanjaro afunguka


Kaimu kamanda polisi mkoani Kilimanjaro, Ronald Makona alisema ajali iliyosababisha kifo cha Jackson na wenzake ilitokea saa 12:00 asubuhi eneo la Shah Tours baada ya kugongwa na gari aina ya Toyota Coaster.


“Ajali hiyo ilisababisha kifo cha Phidelis Leonard Moshi (29) ambaye ni mwalimu huko wilaya ya Rombo na kusababisha majeruhi wawili ambao ni Jackson na Emanuel Mandara (29) ambaye naye ni mwalimu pia,” alisema.

Majeruhi hao nao walifariki wakitibiwa Hospitali ya Rufaa ya Mawenzi.

“Dereva wa Coaster alitoroka baada ya ajali. Uchunguzi zaidi unaendelea pamoja na kumsaka dereva aliyesababisha ajali hiyo,” alisema Makona jana.


Katika ajali nyingine iliyotokea eneo la KDC Mjini Moshi, Desemba 31 na kusababisha kifo cha George Washington, Makona alisema anafuatilia kujua chanzo.

Marafiki washtushwa


Hata hivyo ndugu, jamaa na marafiki walisema ajali hiyo ilitokea saa 8:00 mchana wakati George akiendesha pikipiki kutoka Kwa Alfonsi kuelekea KDC ambako ni jirani na alikokuwa anaishi.

Vick Mushi, jirani wa marehemu alisema wameelezwa kuwa George aligongwa na daladala na kujeruhiwa vibaya kichwani.


“Tulivyoelezwa ni kuwa alipogongwa na hiyo Hiace (daladala) alikimbizwa Mawenzi na baadaye KCMC ambako alifanyiwa upasuaji kichwani lakini jana (juzi) alifariki dunia. Ni msiba umetuumiza sana,” alisema.


Kwa upande wake, rafiki wa karibu wa Jackson, Victor Mjema alisema aliachana naye saa 7:00 usiku baada ya kuupokea Mwaka Mpya wakiwa Kili East Park na alishtushwa na taarifa asubuhi kuwa amefariki dunia.

“Ni msiba ambao sidhani kama nitausahau kwa sababu nilikuwa naye mpaka saa 7:00 usiku na tukapokea mwaka mpya pamoja. Alikuwa mcheshi, mwenye nidhamu na alipendwa na kila mtu,” alisema.


Dada wa marehemu Jackson aitwaye Hellen Kisamo alisema msiba huo umewashtua na kuwaumiza, wamepanga kuzika Jumanne ijayo nyumbani kwake Mdawi.


Wasifu wa marehemu

George Jamal, ni mfanyabiashara anayemiliki malori na nyumba za kupanga katika eneo hilo la KDC.

Kutokana na kuendesha pikipiki kubwa ilimlazimu kila aliyekutana naye barabarani aitizame mfanyabiashara huyo mcheshi anayependa kujichanganya na watu kulimfanya awe mashuhuri mjini hapa.

Jackson Kisamo alikuwa akisambaza vinywaji kutoka duka kubwa la jumla lililopo eneo la Mdawi.

Baada ya kumaliza shahada yake Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (Muco) alijishughulisha kazi hiyo pamoja na kuhudumia wageni wanaopanda Mlima Kilimanjaro.

Ni mtu aliyekuwa akifahamika sana kwa makundi ya vijana kutokana akiitwa kwa jina la utani la “Mkata Umeme” alilopewa kutokana na umahiri wake katika kulisakata kabumbu.

Phidelis Leonard Moshi (29) yalikuwa mwalimu wilayani Rombo kama ilivyo kwa Emannuel Sadick Mandara anayefundisha Shule ya Msingi Ilonga iliyopo Kilosa mkoani Morogoro.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad