Wadaiwa Sugu Wa Ardhi Sasa Kufutiwa Umiliki Kwa Mujibu Wa Sheria

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





Na Munir Shemweta, WANMM SIMIYU
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewaagiza Maafisa Ardhi katika halmashauri nchini kuanza kuwafutia umiliki wa ardhi wadaiwa wote sugu wa kodi ya pango wa ardhi kwa mujibu wa sheria. 

Mmiliki yeyote wa ardhi anapaswa kulipa kodi ya pango la ardhi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa masharti ya umiliki kwa mujibu wa kifungu 33 (1) cha sheria ya ardhi Na 4 ya mwaka 1999.

Aidha, kifungu cha 48(1) (g) kinaelekeza kuwa kodi ya ardhi isipolipwa kwa kipindi cha miezi sita mara baada ya mmiliki kutumiwa ilani ya madai mmiliki huyo anaweza kufutiwa milki yake.

Akiwa katika ziara yake ya siku moja katika mkoa wa Simiyu tarehe 25 Januari 2021 kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya pango la ardhi na kuzungunza na watendaji wa sekta ya ardhi, Naibu Waziri wa Ardhi aliwaelekeza wataalamu wa sekta ya ardhi kuhakikisha wanatekeleza matakwa hayo ya kisheria Na 4 ya mwaka 1999 kwa kuisimamia vyema.

“Nawaagiza Maafisa Ardhi katika halmashauri zote kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake na msiendelee kuwalea wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi na mzingatie sheria Na 4 ya ardhi wakati mnatekeleza majukumu yenu ikiwemo kufuta umiliki baada ya miezi sita kwa wadaiwa” alisema Dkt Mabula.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula aliwataka Wakurugenzi katika halmashauri za mkoa wa Simiyu kuzitumia vyema idara za ardhi katika masuala yote yanayohusu ardhi ikiwemo upangaji wa miji kwa kuwa mamlaka za upangaji ziko chini ya halmashauri hizo na kusisitiza kuwa wakurugenzi hao wasipozitumia vyema idara za ardhi kuna hatari ya kuendelea kwa ujenzi holela.

Aidha, Dkt Mabula ameonesha kutoridhishwa na kasi ndogo ya ukusanyaji kodi ya pango la ardhi katika mkoa wa Simiyu ambapo hadi sasa mkoa huo umekusanya shilingi 87,654,120 sawa na asilimia 24 huku mkoa ukidai zaidi ya Bilioni 5.5 kutoka kwa wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi.

Kwa upande wake Kamishna Msaidizi wa Ardhi katika mkoa wa Simiyu Essau Mwakatumbula alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi Dkt Mabula kuwa ofisi yake itahakikisha inaongeza kasi ya kufuatilia wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi ili iweze  kukusanya madeni na kufikia malengo ya makusanyo ya kodi ya ardhi iliyojiwekea.

Hata hivyo, alisema pamoja na jitihada za mkoa katika kuhakikisha wadaiwa wote wa kodi ya ardhi wanalipa kuna changamoto kwa baadhi ya taasisi kutoonesha jitihada zozote za kulipa na kutolea mfano wa VETA, SIDO na SHIRECU.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hapa kuna utata wa uwajibikaji. ikiwa watu wamemilikishwa Ardhi na hati bado zippo wizarani au mahali husika na aliemilikishwa hajui lini ataitwa kupokea hati yake watu wamezilalia hati miliki ofisini kwa si ajabu miaka
    SI NDIOUTENGENEEZAJI WA MAZINGIRA YA DHULUMA..??

    HILI MKAE CHINI NA TIMU ZENU MLICHAMBUE IPASAVYO MABULA NA HATUA KAZI ZICHUKULIWE KULINDA HAKI ZA WANYONGE NA WAFU KWA FAMILIA ZAO.

    LUKUVI AMELIONA NA ANALIJUA HILI HASA ARUSHA DODOMA NA MOROGORO.

    ReplyDelete

Top Post Ad