Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Walimu Wamtoa Mimba Mwanafunzi, Wadakwa na Polisi

 


Na Amiri Kilagalila,Njombe

Jeshi la polisi mkoani Njombe linawashikilia walimu wawili wa shule ya sekondari Mang’oto wilayani Makete mkoani Njombe,kwa tuhuma za kumsababishia ujauzitoa na kumtoa mwanafunzi wa shule hiyo mwenye umri wa miaka 17.


Akizungumza na vyombo vya habari,kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa,amesema wanamshikilia mwalimu Ezekiel Thomas (36) maarufu kwa jina la Dokole,kwa kuwa na mahusiano na mwananfunzi na kumsababishia ujauzito.


“Huyu mwalimu amekuwa na mahusiano na mtoto wa sekondari mwenye umri wa miaka 17 na binti huyo amepimwa  amegundulika ni mjamzito”alisema kamanda Issa


Aidha amesema wanamshikilia mwalimu Ben Liamdilo (35) kwa kushirikiana katika tukioa la utoaji wa mimba na kumsababishia maumivu mwanafunzi.


“Mwalimu Thomas alifanya juhudi akamtuma huyu mwalimu mwenzake akambeba na boda boda kwenda kumtoa mimba mpaka sasa hivi walimu wote wawili tunawashikilia na wanatuhumiwa na makosa haya”alisema tena kamanda Issa


Vile vile ameitaka jamii kushirikiana kwa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi ili kukabiliana na vitendo kama hivyo.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments