Wanachuo 13 Mbaroni kwa Udanganyifu Mtihani wa ‘Sup’

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Dodoma inawashikilia wanafunzi 13 wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) cha jijini Dodoma kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa na udanganyifu wakati wa kufanya mtihani.

 

Imedaiwa kwamba wanafunzi hao kwa kutumia rushwa waliweza kurudia kufanya mtihani nje ya chumba cha mtihani na baadaye walijaribu kuingiza karatasi za kujibia mtihani kwenye mfumo rasmi ambapo chuo kiliwabaini na kutoa taarifa Takukuru.

 

Hayo yameelezwa leo Januari 16, 2021, na Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Dodoma, Sostenes Kibwengo, wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya utendaji wa Takukuru mkoa huo kwa robo ya Oktoba hadi Desemba mwaka 2020.

 

Amesema wanawashikilia wanafunzi hao wa mwaka wa tatu kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa na udanganyifu wakati wa kufanya mtihani wa marudio (supplementary examination) wa somo la Applied Statistics II uliofanyika Novemba mwaka jana chuoni hapo.

 

Ameongeza kwamba uchunguzi wa awali umeonyesha kwamba wanafunzi hao, kwa kutumia rushwa, walirudia kufanya mtihani huo nje ya chumba cha mtihani na baadaye walijaribu kuingiza karatasi za kujibia mtihani kwenye mfumo rasmi ambapo alidai chuo kiliwabaini na kutoa taarifa Takukuru.

 

Pia amewataka waliokuwa wanafunzi wa chuo hicho, Evarist Nyaki na Lameck Kawinga, kuripoti mara moja kwenye ofisi za Takukuru Mkoani Dodoma kwa ajili ya kusaidia uchunguzi huo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad