Watoto wa familia moja wapoteza maisha

advertise here

 


Watoto wawili Ashiri Malimi(4) na Laurencia Malimi (2), wakazi wa kata ya Kaseme mkoani Geita, wamefariki dunia huku wengine saba wakinusurika baada ya kuangukiwa na  ukuta wa nyumba, ulioanguka kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha mkoani humo.

 

Taarifa hiyo imetolewa leo Januari 26, 2021, na Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe, na kusema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo.


"Hawa watoto wameangukiwa na ukuta wa nyumba yao na kufariki dunia, nawaomba tu wananchi wawe na tahadhari kwa watoto wao na familia katika kipindi hiki cha mvua na kila mtu anajua uimara wa nyumba yake", amesema Kamanda Mwaibambe.


Kwa upande wake Baba wa watoto hao Malimi Kiswetura, amesema kuwa tukio hilo limetokea maira ya saa 2:00 usiku na wakati ukuta unaanguka yeye hakuwepo nyumbani, na kwamba alikimbiliwa na mtoto mwingine na kumuambia kwamba watoto wake wameangukiwa na nyumba.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE