Watu 14 Mbaroni kwa Kuiba Korosho za Mil 160

Polisi mkoani Mtwara linawashikilia watu 14 kwa tuhuma za kula njama, kuvunja Ghala la Korosho na kuiba gunia za korosho 1,515 zenye thamani ya zaidi ya Tsh. Milioni 160.

 

Kamanda wa Polisi mkoani Mtwara, Mark Njera amesema, watuhumiwa tisa wamefikishwa Mahakamani kwa la kuiba korosho, huku watuhumiwa watano wakishikiliwa kwa kosa la kupatikana na korosho zisizo na ubora.

 

Kabla ya watuhumiwa kufikishwa Mahakamani walikiri kufanya kosa hilo ambapo kabla ya tukio walinzi wawili waliacha kazi ghafla bila kutoa taarifa kwa viongozi wao na walipohojiwa walikiri kushiriki wizi huo.

 

Aidha, baadhi ya wanaoshikiliwa kwa kukutwa na gunia mia moja zisizo na ubora ni Viongozi wa Chama cha Msingi cha Mwembe Tongwa.

 


That Gal ya Rosa Ree Yawa Gumzo Itazame Hapa chini:

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments