Watu 5 wakutwa wamefariki ndani ya nyumba Marekani
Watu 5, mmoja wao akiwa mjamzito wamepatikana wamefariki kwenye nyumba moja iliyoko katika mji wa Indianapolis nchini Marekani.

Mamlaka ilitangaza kuwa hapo jana karibia saa 4:00 za asubuhi, timu ya maafisa wa polisi ambao walikwenda eneo la tukio baada ya kupokea taarifa, walipata miili ya watu 5 katika nyumba moja mjini Indianapolis.

Taarifa zilifahamisha kuwa watu 5 walipatikana wakiwa wamefariki nyumbani humo, mmoja akiwa ni mjamzito.

Iliarifiwa kwamba mwanamke mjamzito alipelekwa hospitalini lakini mtoto hakuweza kuokolewa.

Ripoti ya maafisa wa polisi ilibainisha chanzo cha vifo vya watu hao kilitokana na majeraha ya bunduki.

Uchunguzi umeanzishwa juu ya tukio hilo.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE