Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Wawili wakutwa na COVID-19 Barcelona
Klabu ya Barcelona ya nchini Uhispania imethibitisha kuwa maafisa wake wawili wamekukutwa na COVID-19 usiku wa kuamkia leo Januari 5, 2021, baada ya kufanyiwa vipimo kuelekea mchezo wao wa ligi kuu 'La Liga' dhidi ya Athletic Bilbao unaotaraji kuchezwa kesho saa 5:00 usiku tarehe 6 Januari
Taarifa hiyo imeeleza kuwa “Baada ya vipimo vya PCR vilivyofanywa jumatatu, maafisa wetu wawili kutoka kwenye timu ya wakubwa (ambayo ni Barcelona) wamekutwa na COVID-19”.

“Klabu imewajulisha mamlaka husika za michezo na Afya, vilevile kikosi chote kitafanyiwa vipimo vya PCR zaidi siku ya jumanne asubuhi (leo) kutokana na utaratibu mpya wa kujikinga na COVID-19”.

“Kutokana na hilo, muda wa kufanya mazoezi uliopangwa leo na zoezi la kuzungumza na wanahabari kuelekea kwenye mchezo wetu wa la liga dhidi ya Athletic Bilbao pia limeghairishwa na muda mwingine utapangwa kesho”.


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments