1/15/2021

Waziri Aweso Asitisha Agizo la EWURA Kupandisha Ankara za MajiWaziri wa Maji Mheshimiwa Juma Aweso amesitisha zoezi lililokuwa likiendelea kwa agizo la Mamlaka  ya Udhibiti wa  Maji na Nishati(EWURA) la kuzitaka mamlaka za maji nchini kupandisha ankara za maji  mpaka hapo atakapojiridhisha na  kuruhusu utaratibu huo kuendelea.

Download App ya Udaku Spesho HAPA

Waziri Aweso ametoa maagizo hayo jijini Dodoma wakati akifungua kikao  kazi cha siku mbili cha wizara ya maji na Taasisi zake ambapo amesema bado hajaridhika na kazi zinazofanywa na mamlaka  hiyo katika eneo la udhibiti katika utoaji wa huduma za maji huku akiwataka kujipanga zaidi. 


"Ninyi EWURA hamjaweza kutusaidia katika mambo hayo yote, jukumu lenu si kuelekeza mamlaka kupandisha bei za maji tu, bali mnawajibu pia wakusimamia na kutatua kero za wananchi katika suala zima la utoaji huduma za maji," amesema Mhe Aweso.


Aidha amebainisha kuwa kumekuwa na changamoto kubwa ya ubambikiwaji wa ankara kwa wananchi kuna wakati wananchi wanaadhibiwa mahali ambapo hawakustahili kuadhibiwa.


Amesema kwa mda sasa wamekuwa wakipokea malalamiko ya ubambikiziwaji Ankara za maji kwa wananchi, jambo hilo hata Rais, Dk. John Magufuli alishawahi kulizungumzia na kuonyesha kukerwa nalo, sitokubali jambo hilo kuendelea lazima tuwatendee haki wananchi.


Amewaagiza EWURA kukagua na kuanisha mamlaka zote ambazo ni vinara katika kubambikizia wananchi ankara za maji ambazo hawakupaswa kulipa katika matumizi yao ya maji.


Awali Naibu Waziri wa Maji Mheshimiwa Maryprisca Mahundi, amesema kuwa miradi mingi inayofanya kazi nchini imepitwa na wakati hivyo kuna haja ya kufanya taratibu na Mipango ya kuiboresha kutokana na uchakavu wa miundombinu na vifaa.


Naibu Waziri huyo amewataka wataalam kufanya mapitio upya katika miradi hiyo nchi nzima na kuwasilisha taarifa ya namna ya kuikarabati na bajeti nzima itakayohusika kwa ajili ya maboresho.


Amesema kumekuwa na changamoto kubwa katika utekelezaji wa miradi ambayo imekamilika kutokana na jumuiya nyingi za maji kutofanya vizuri katika usimamizi mara baada ya kukabidhiwa miradi hiyo.


Naibu Waziri Maryprisca amesema pia kumekuwa na changamoto ya miradi mingi kutokamilika ili hali akaunti za mameneja zina fedha, jambo hili linasababishwa na mameneja kutojiamini au kukosa kibali cha kutekelezeka majukumu yao kutoka kwa viongozi wa juu.


Naye Naibu katibu mkuu wa wizara Maji, Nadhifa Kemikimba amesema hivi sasa kuna changamoto kubwa katika usimamizi wa vyanzo vya maji kutokana na shughuli za kilimo, ufugaji na uchimbaji madini na shughuli nyingine zinazofanywa na binadamu.HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger