Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Waziri wa Afrika Kusini apatikana na corona
Waziri Jackon Mthembu alikuwa na maumivu ya tumbo kabla ya kupimwaImage caption: Waziri Jackon Mthembu alikuwa na maumivu ya tumbo kabla ya kupimwa
Waziri wa nchi katika ofisi ya rais Jackson Mthembu amekuwa waziri wa nne katika serikali ya Afrika Kusini kupatikana na virusi vya corona.

Bw Mthembu alipimwa virusi hivyo baada ya kuwa na dalili, ilisema ofisi ya rais.

Amewekwa katika karantini pamoja na kila mtu aliyekaribiana naye

Waziri Mthembu alitweet akisema ana maumivu ya tumbo :

Afrika Kusini ina aina mpya ya virusi vya corona inayosambaa kwa kasi kubwa.

Nchi hiyo ilirekodi wagonjwa wapya 15,046 na vifo vipya416, na kulifanya taifa hilo kufikia jumla ya wagonjwa wa corona1,246,643 na vifo 33,579.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments