Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Yanga Yawachinjia Baharini Ihefu FCUONGOZI wa Yanga kupitia kamati yake ya usajili, imewachinjia baharini mabosi wa Ihefu FC, kufuatia barua yao ya kumtaka mshambuliaji wao Waziri Junior, akajiunge nao kwa mkopo.

 

Takribani mwezi mmoja sasa Ihefu iliandika barua yake kwa uongozi wa Yanga, ukimuomba Waziri ajiunge na kikosi chao baada ya kusikia wanataka kumtoa kwa mkopo.Akizungumza na gazeti hili, Kocha Mkuu wa Ihefu, Zubeir Katwila ameweka wazi kuwa, pamoja na kuendelea kuaminishwa na uongozi wa Yanga kuwa atapewa saini ya Waziri, amepata habari za ndani kuwa mchezaji huyo huenda akapelekwa Coastal Union ya Tanga.

 

“Nimesikia kuna uwezekano wa kumkosa Waziri, ambaye tuliwaomba Yanga watupatie kwa mkopo tena mapema kabi-sa, nilimtege-mea sana Waziri kuja kutu-saidia ila kama kweli wameamua kutotupatia siyo mbaya, tutajitahidi kuwatumia washam-buliaji ambao tumewapata kipindi hiki,” alisema Katwila

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments