Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Zimbabwe yafunga tena shughuli za kawaida kufuatia ongezeko la covid-19

 


Serikali ya Zimbabwe jana imesitisha shughuli za maisha ya kawaida kote nchini humo kufuatia kuongezeka kwa visa vya maambukizi ya Covid-19, hatua inayowaweka katika hali ngumu raia wake wanaotegemea ajira ya sekta isiyo rasmi. 

Makamu wa Rais na waziri wa afya Constantino Chiwenga amewaambia wanahabari kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa katika msimu huu wa sherehe ambalo liliongeza marudufu idadi ya maambukizi yaliyorekodiwa katika mwaka mzima. 


Ni huduma muhimu pekee, kama vile hospitali, maduka ya dawa na maduka ya jumla yatakayoendelea kuhudumu kwa siku 30 zijazo, hali inayoongeza mbinyo kwa familia ambazo tayari zinakumbwa na umaskini. 


Taifa hilo la kusini mwa Afrika tayari linakabiliwa na mgogoro mkali wa kiuchumi, mfumuko wa bei na kiwango cha juu cha ukosefu wa ajira.


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments