Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Abiria Kenya Airways Ruhusa Kulipia Viti vya Ziada Kujikinga na Corona


ABIRIA wa ndege za shirika la Kenya Airways (KQ) sasa wanaweza kununua kiti cha ziada cha pembeni wakati wanasafiri iwapo wanataka kuwa mbali na abiria wengine.


Huduma hiyo inayoitwa Economy Max itakuwepo kwa watu wanaotaka faragha na usalama hasa wakati huu wa kuenea kwa ugonjwa wa Covid-19.


Wanaotaka kufanya hivyo watalazimika kununua mapema kiti kimoja au zaidi katika muda wa kati ya saa tatu na 48 kabla ya kusafiri.


Abiria wa ndani watalipa Dola 15 kwa ajili ya kiti cha ziada na Dola 20 kwa viwili.

Abiria kutoka au kwenda Nairobi kutoka Amerika watalipa Dola 120 kwa kiti cha ziada na Dola 230 kwa viti viwili.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments