2/06/2021

Alichokisema Billnass kuhusu vyombo vya Nandy
Msanii Billnass amesema kuwa suala la mchumba wake Nandy kusemwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu vyombo vyake alivyotumia kumpakulia chakula Koffi Olomide, kwa upande wake hakuona shida yoyote kwa kuwa yeye hayo mambo hayajui na hajakulia kwenye mazingira hayo.


Billnass ameyasema hayo kwenye Friday Night Live ya East Africa Television, baada ya kuulizwa alichukuliaje suala la mpenzi wake kushambuliwa mitandaoni kuhusu suala la vyombo.

 DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE

"Kiukweli mimi kwa maisha niliyokulia, familia niliyotoka, mitaa niliyokulia kuna vitu vingi sana sivijui, hata haya mambo ya vyombo gani sijui ni vitu ambavyo mimi sijui, nimekua kwenye mazingira ya nyumba ya chumba kimoja kisha viwili kwahiyo hata kuwa na meza na sehemu ya kulia ni ushindi, vyombo siyo vitu navitazamia hata baada ya kuona hivyo nina vitu vinbgi sana vya kuvifikiria kuliko hivyo vitu vidogo vidogo", amesema Billnas
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger