Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Aliyekuwa Mgombea Urais Uganda Bobi Wine Ndio Sababu ya Tuzo za MTV Mama Kuhairishwa Afunguka "MTV Walikuwa Wanatumika Kuhalalisha Utawala wa Kinyonyaji"

 


Waandaaji wa tuzo za (MTV MAMA 2021) wameahirisha hafla za ugawaji wa Tuzo hizo za 7 zilizokuwa zifanyike Kampala Uganda Februari 20 mwaka huu.


Kwenye taarifa yao, MTV Base wamesema wameahirisha ugawaji wa tuzo hizo mpaka itakapo tangazwa tena huku wakishindwa kutaja sababu iliyopolekea.


Tovuti ya CNN imeripoti kwamba Bobi Wine na wafuasi wake wanahusika kwenye sababu za MTV MAMA 2021 kuahirishwa kutokana na madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na serikali ya Uganda, madai ambayo yamewasilishwa mtandaoni na Bobi Wine ambaye alikuwa mgombea wa Kiti cha Urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.


 DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE

"Ilikuwa ni maumivu makali kuona MTV walikuwa wakitumika kuhalalisha utawala wa kinyonyaji hapa Uganda. Nimefurahi kuona MTV wameona hili na kuchukua hatua kwa ajili ya kuheshimu haki za wasanii wote. Ingekuwa ni aibu kwa MTV Music Awards kufanyika hapa Uganda chini ya mtutu wa bunduki." alisema Bobi Wine jana Alhamis kwenye mkutano na waandishi wa habari.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments