Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Amber Lulu: Pigeni Kelele, Nasubiri KujifunguaAMBER Lulu ni bonge moja la msanii wa Bongo Fleva ambaye alianza kama muuza sura (video queen) kwenye video. Alianza kupata umaarufu baada ya kupiga picha za utupu na kuzisambaza mitandaoni huku Serikali ikishindwa kumchukulia hatua kutokana na kutokuwepo kwa sheria za kumbana wakati huo.

 

 

Amber Lulu anasema maisha yake ya nyuma yalikuwa yenye sarakasi nyingi akiwa na umri mdogo ambapo alilazimika kujitafutia hadi pesa ya shule.

 

 

Anasema wakati akiwa mdogo akisoma, mama yake alikuwa na tatizo na lililomfanya ashindwe kutimiza majukumu mengi ya kifamilia, hivyo akaamua kujiingiza kwenye masuala mbalimbali ya kujitafutia riziki ili aweze kumudu gharama za maisha.

 

 

Itoshe kusema kwamba unapozungumzia wasanii ambao wamepigana vilivyo mpaka kufikia hatua aliyopo bila kujali Dunia itawaonaje, basi mwanadada Amber Lulu anaweza akawa kwenye tano bora.

 

 

Leo amekuwa ni msanii mzuri wa Bongo Fleva akiwa na sifa ya ziada ya kuweza kumiliki vyema jukwaa.

Jina lake halisi ni Lulu Euggen ambaye kwa sasa ni mjamzito.

 

 

Katika mahojiano maalum (exclusive interview) na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, Amber Lulu anasema kuwa, watu wengi wanamshangaa na kuona amebeba ujauzito ni kama kitu cha ajabu au kimewashangaza hivyo anawaomba watulize kelele kwanza, yeye anasuburi kujifungua mtoto wake kisha maisha yaendelee. Amber Lulu, alizungumza hayo alipokuwa akifanya mahojiano na Ijumaa Wikienda kama ifuatavyo:Wikienda: Habari Amber,na hongera naona mambo ni mazuri

Amber Lulu: Asante, Mungu akipanga lake amepanga kwakweli.

Wikienda: Ila umejificha sana watu wengi walikuwa hawajui kama ni mjazito, kwanini umejificha hivyo?

 

 

Amber Lulu: Macho ya watu nayaogopa kwasababu kipindi kama hiki lazima usiweke kila kuitu kwenye mitandao kwasababu hujui nani mzuri kwako,hivyo niliamua kujikalia tu.

Wikienda: Maana huko mitandaoni kila mtu anaongea lake na kutaka kujua baba wa mtoto.

 

 

Amber: Jamani hebu waniache nizae zangu,kelele wazipeleke huko mbele kwasababu hata wakimjua baba wa mtoto watanisaidia kuleta nepi au maziwa, lakini pia itawasaidia nini.

Wikienda: Unajua mastaa wengi wamekuwa na tabia ya kuwaweka wazi wapenzi wao na hata wewe kipindi cha nyuma ulikuwa unafanya hivyo sasa hapa nashangaa kwanini?

 

 

Amber: Kila kitu kinabadilika kutokana na mazingira,lakini pia nimejifunza mengi sana kuhusiana na kuweka wapenzi mitandaoni na tulikuwa hatujui tu kuwa hayo ni maisha binafsi ya mtu,tulikuwa tunakosema sana, mii hayo mambo sipendi kabisa,wasubiri tu mtoto watamuona kwasababu sio wa kuficha.

 

 

Wikienda: Sasa hivi huko kwenye hali hiyo,na ukiangalia maisha yako unategemea muziki kwa maana ufanye shoo ili chochote kiingie kinywani, hii inakuaje?

 

 

Amber: Nikipata shoo nafanya tu mbona kwasababu, hakuna kinachonizuia kabisa,kwasababu kuna wengine wanapanda jukwaani kuimba, wakishuka wanaenda kujifungua basi hata mimi napiga kazi kama kawaida hakuna shida maana mimi nimpambanaji toka kitambo sana.

 

 

Wikienda :Hivi ulishawahi kuzaa mtoto huko nyuma,au huyu utakayejifungua ndio kwanza?

Amber: Huyu Mungu, akinisaidia kujifungua salama ndio mtoto wa kwanza sikuwahi kuzaa mwingine kabla, wala sijawahi kuficha mtoto kama watu wengine wanavyofanya.

 

 

Wikienda: Ungependelea upate mtoto gani?

Amber: Mimi yeyote tu ambaye mwenyezui Mungu,atanichagulia nitashukuru.

Wikienda: Ni kitu gani ambacho utokipenda mtoto wako asikione akija kuwa mkubwa kuhusu wewe?

 

 

Amber: Kwanza kabisa natamani akikua asikute mitandao ya kijamii hii,tuliopitia wala asijue kilichowahi kutokea kuhusu mimi huko nyuma,yaani sitaki kabisa.

Wikienda: Haya asante sana Amber.

Amber: Shukurani sana.


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments