Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Antonie Nugaz "Tambeni Mtaani Msitembee Kinyonge, Vimbeni Mtaani Kombe Tunachukua"

 


Afisa Muhamasishaji na msemaji wa klabu ya Yanga SC Antonie Nugaz amewatoa hofu mashabiki wa timu kutokana na matokeo waliyoyapata kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City.

Kupitia taarifa aliyoitoa Nugaz amesema ''Mwanachama, mpenzi na shabiki wa Yanga Kwanini ukajikosesha amani kwa timu kutoka sare na kuaminishwa Kuwa timu haitopata matokeo na wewe unaamini hilo.


Kumbuka mpaka sasa tuko kileleni (Namba moja) kwenye msimamo wa ligi na pia tukiwa na rekodi sahihi ya kutopoteza Mchezo hata mmoja.


Lazima tukubaliane na matokeo ya Mpira na sio kulaumu sana kana kwamba tuko nafasi ya 8 au tunaburuza mkia.


Tambeni Mtaani msitembee kinyonge,vimbeni mtaani na muendelee kuipa hamasa timu yetu Insha Allah kila kitu kitaenda Sawa.


Kisha tukutane Uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya jumatano kwenye Mchezo wetu dhidi ya Kagera Sugar saa 1 Kamili usiku Tujitokeze kwa wingi bila kukosa.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments