2/15/2021

Baba mzazi wa rapa Nicki Minaj Agongwa na Gari na Kufariki, Aliyemgonga Akimbia


 Baba mzazi wa rapa Nicki Minaj, Robert Maraj amefariki dunia mara baada ya kugongwa na gari.

Rpbert Maraj alikuwa akitembea pembezoni mwa barabara Mineola, mjini New York siku ya Ijumaa (Feb. 12) ambapo aligongwa na gari ambalo halikusimama baada ya kutekeleza ajali hiyo. Taarifa ya polisi wa kitongoji cha Nassau wanasema dereva alifanikiwa kukimbia na bahati mbaya hakukuwa na shuhuda yoyote kwa ajili ya kutoa maelezo.

 DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE

Mzee huyo aliyekuwa na umri wa miaka 64 alikimbizwa hospitali akiwa na hali mbaya ambapo alitangazwa kuwa amefariki siku ya Jumamosi. Polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger