Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Boss Haji Manara-Star Mkubwa kuwahi kutokea katika soka

 


Afisa habari wa Simba SC Haji Manara maarufu kama De La Boss ni moja kati ya watu maarufu sana katika michezo kwa sasa.


Haji sio tu ni maarufu katika michezo bali ametokea katika familia ya mpira, kingine kilichomfanya Haji Manara kuwa maarufu sana ni hali yake ya kujiamini zaidi ukilinganisha na hali yake ya ulemavu wa ngozi ‘Albino’ ambapo wengine huwa wanajitenga na kuhisi kama ndio basi tena kwenye haya maisha.


Baba mzazi wa Haji Manara anasema kijana wake alianza kujiamini tangia utotoni na amewahi kumletea mashekh nyumbani na kumuamsha na kumshitaki kwa mashekh kuwa baba yangu mimi hasali.


Kwa jicho langu Haji Manala sio tu analiweka soka kwenye ushindani mkubwa bali amekuwa star wa kwanza kuvuma sambamba na mastar wa entertainment huku yeye akitokea upande wa soka. Leo hii ndani ya dakika 10 kurusa mitandao za Haji huwa na comments zaidi ya 200 pale anapopasha habari.


Hongera semaji la dunia. Nakutakia maisha marefu

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments