Breaking: Katibu Tawala wa Arusha Afariki Ajalini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





Katibu tawala Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega.

KATIBU tawala Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega amefariki katika ajali ya gari leo Jumatano Februari 3, 2021 wakati akitoka mkoani humo kwenda Dodoma baada ya gari alilokuwa amepanda kugongana na basi.

 

Akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joseph Mkirikiti amesema ajali hiyo imetokea eneo la Mdori Mizani, Babati.

 

Amesema katika ajali hiyo watu wengine wanne wamejeruhiwa ambao ni dereva wa katibu tawala huyo na wanawake watatu waliokuwa kwenye basi.

“Ni ajali mbaya kumpoteza katibu tawala na muda huu tunajiandaa kurejesha mwili Arusha bado tupo kituo cha afya hapa Magugu,” amesema.



Amesema majeruhi wanaendelea vizuri na wamehamishiwa hospitali ya Mkoa wa Manyara.

Basi lililogongana na gari la katibu tawala huyo lilikuwa linatoka Singida kwenda Arusha.

Leo asubuhi Kwitema alimwakilisha katibu mkuu wa Wizara ya Fedha, Dotto James kwenye mkutano wa wizara hiyo na wahariri wa vyombo vya habari kuhusu uboreshaji wa mfumo wa kielektroniki wa malipo serikalini (GePG) uliofanyika mjini Arusha

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad