Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Breaking News: Askofu Mwamakula wa Kanisa la Uamsho la Moravian Akamatwa DarJeshi la Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam leo tarehe 15.02.2021 limefanikiwa kumkamata anayejiita Askofu EMMAUS BANDEKILE MWAMAKULA wa kanisa la Uamsho la Moravian kwa kosa la kuhamasisha maandamano nchi nzima kwa njia ya ujumbe wa maneno katika mitandao ya kijamii. 

Taarifa ilikuwa ikihamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi ili kuandamana wakishinikiza na kudai katiba mpya jambo ambalo ni kinyume na taratibu na sheria za nchi.


Aidha awali Jeshi la Polisi kupitia idara ya upelelezi kanda Maalum Dar es salaam walifanikiwa kupata taarifa hiyo na kumkamata Askofu huyo kwa ajili mahojiano kwa jambo hilo ambalo lilileta taharuki kwa umma katika mitandao ya kijamii.


Jeshi la Polisi linatoa onyo kwa yeyote ambaye ameshawishika na kupanga kuandamana kuahirisha mara moja nia hiyo ovu ambayo iko kinyume na sheria.


Pia ifahamike ni kosa kufanya maandamano bila kuwa na kibali cha Polisi ili kupewa ulinzi, na atakayejaribu kuandamana atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria. Hivyo wananchi wote wa jiji la Dar es salaam waendelee na shughuli zao za kukuza uchumi na kujipatia vipato vyao vya kila siku.


LAZARO B. MAMBOSASA– SACP

KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM

DAR ES SALAM.

15.02.2021

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments